Wednesday, June 10, 2015

Wanamtandao

Katika picha hapo juu ni ya Wanamtandao amabao wameunganishwa na Shirika la 2SEEDS Network ambao wamo katika vikundi tofautitofauti kutoka katika miradi mbalimbali ipatayo nane na ambayo imesambaa katika vijiji mbalimbali vilivyomo katika wilaya ya Korogwe Vijijini. Vijiji hivyo ni hivi vifuatavyo Kwakiliga,Tabora,Magoma, Magoma Kwata, Bombo Majimoto,Kijungumoto,Lutindi na Bungu.

Katika vijiji hivyo kuna miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kama vile ufugaji nyuki,kuku na mbuzi na kilimo cha mazao mbalimbali.

Tutakuwa tunawaletea taarifa za mradi mmojammoja kila siku hadi mwisho.

Wanamtandao wa 2SEEDS Network - Korogwe Vijijini

 Katika picha hapo juu ni sehemu ya bwawa la samaki, na banda la kuku ambalo limejengwa ndani ya eneo la bwawa kama linavyoonekana hapo katika picha. Miradi hii miwili inategemeana kiutunzaji kwani mbolea inayotokana na kuku katika banda hudondokea ndani ya bwawa la samaki na kuwa chakula cha samaki. Miradi hii ipo katika kijiji cha Magoma Kwata wilayani Korogwe vijijini,lakini pia miradi hii iliyobuniwa na Wanamtandao wa 2Seeds Network ipo chini ya uangalizi wanamtandao wa Shule ya Msingi Kwata.

 Katika picha hapo juu ni banda la kuku likwa na kuku ndani yake na tayari mradi huu umeanza kuzalisha mayai,mojawapo ya miradi iliyopo katika Kijiji cha Magoma Kwata unaosimamiwa na baadhi ya Wanafunzi wa Shule hiyo ya Kwata ambao wameunganishwa katika Mtandao wa 2SEEDS Network.

 Katika picha hapo juu ni mradi wa Vitunguu saumu ambao naoupo katika kijiji cha Magoma Kwata,wanamtandao waliopo katika kikundi hiki hutumia drip irrigation method katika kumwagilia mimea ya vitunguu katika matuta yake kama inavyoonekana mipira hiyo midogomidogo imetandazwa kwa kufuata mistari ya mimea.

 Katika picha hapo juu aliyesimama wapili kutoka kulia ni Bwana Vedastus Valentine ambaye ni Afisa Biashara kutoka Shirika la Masoko Kariakoo akiwa anamsikiliza mwanakikundi anaejulikana kwa jina Babu Francis  Mwamkai aliyeshika miwani mkononi mwake akitoa maelezo jinsi wanavyojitahidi kuenedesha miradi yao kwa umakini ili waweze kufikia malengo yakufikia maisha bora.

Katika picha hapo juu ni Mradi wa mbuzi wa maziwa ambao pia upo katika Kijiji hichohicho cha Magoma Kwata, tayari mradi huu umeanza kutoa matunda kwakutoa maziwa. maziwa hayo yanatumiwa na wanafunzi katika kuboresha afya zao,lakini kwa mujibu wa maelezo ya babu Francis Mwamkai wanao mpango wa kuongeza idadi ya mbuzi hao katika kuhakikisha kuwa mradi huo unawaletea tija zaidi.