Monday, February 16, 2015

TUICO-Tawi laShirika la Masoko Kariakoo wapata Uongozi mpya

 Katika picha hapo juu ni Viongozi waliosimamia zoezi la uchaguzi uliowezesha kupata viongozi wapya watakaliongoza Tawi hili katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka huu. Kutoka kushoto ni Bwana Ibrahim Masha ambaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa ambaye pia ni mtumishi katika Shirika la Masoko, Bwana Godwin Mrosso amabaye ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ambaye huyu alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, wengine ni Bwana Willy Kibona ambaye ni Katibu wa TUICO mkoa wa Ilala  na Bi.Maria John Bange yeye ni Mkuu Msaidizi  wa Idara yaWanawake TUICO Mkoa wa Ilala.Hapo walikuwa wakimalizia kujumlisha kura.
 Sehemu ya Wanachama wa TUICO Tawi ,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo wakiwa katika hali ya kusubiria matokeo ya uchaguzi yatangazwe na Wasimamizi wa uchaguzi huo.Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Baadhi ya Wanachama walioshiriki katika uchaguzi  wakiwa wamesimama nje ya Ukumbi mara baada ya kumaliza kupiga kura za kuwachagua viongozi wa Tawi hilo kuanzia ngazi ya Mwenyekiti,katibu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.
 Katika picha ni Bwana Willy Kibona ateteta jambo na Mjumbe wa TUICO Taifa  Bwana Ibrahim Masha ambaye katika picha hayupo na kulia kwake ni Bi.Maria John Bange wote kwa pamoja walifika kusimamia shughuli nzima ya Uchaguzi huo.
 Katika picha hapo juu ni Bwana Ibrahim Masha Mjumbe wa TUICO Taifa akiwa tayari kabisa kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya zoezi la kuhesabu kura.
 Wanachama wakiwa wametulia kabisa wakisikiliza matokeo ya uchaguzi waliokuwa wameufanya .
 Bwana Ibrahim Masha akitanganza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura na kuhesabu.

 Katika picha hapo juu ni dada ambaye alipendekezwa kufanya sala maalum kwa nia ya kumshirikisha  Mungu katika shughuli nzima ya uchaguzi huo.
 Pia katika picha hii hapo juu ni Mzee Idd Mrope nae pia alipendekezwa kufanya Dua maalum kwa ajili uchaguzi huo wakuwapata viongozi bora katika tawi la SMK.
 Wanachama wakiwa wanaimba na kufurahia mara baada ya kumalizika kwa uchagauzi na matokeo kuwa yametangazwa rasmi. Katika uchaguzi huo Bwana Denis Mfuruki alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TUICO Tawi wakati  katika nafasi ya Katibu Bwana Henry Rweijuna aliibuka mshindi.

Katika picha hapo juu ni sehemu ya wanachama wakitoka ukumbini mara baada ya uchaguzi kumalizika, wakiwa wenye nyuso za furaha kwa kuwapata viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano.