Thursday, May 14, 2015

Mkutano wa Baraza kuu la Wafanyakazi

 Hapo juu katika picha ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko kariakoo Bwana Florens Seiya akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi hapo jana mapema asubuhi. Mkutano huo ulifanyika katika kumbi wa mikutano wa Shirika .

 Katika picha hapo juu kutoka kushoto ni Bi.Matha Mnzava kutoka TUICO Mkoa wa Ilala, wapili ni Bwana Ibrahim Masha ambaye ni Katibu wa Baraza  la Wafanyakazi katika Shirika la Masoko, wa mwisho ni Bi.Emy Rweyendera kutoka Baraza la Usuruhishi -CMA, wote kwa pamoja wakiendelea kuratibu shughuli za mkutano huo ndani ya Ukumbi wa Shirika la Masoko Kariakoo.

 Katika picha hapo juu ni Bi.Emy Rweyendera akitoa semina fupi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wajumbe wawakilishi wa wafanyakazi katika baraza kuu la wafanyakazi katika Shirika la Masoko Kariakoo.Bi.Rweyendera ni Mtumishi kutoka CMA alikuja kusimamia uchaguzi huo.

 Bi.Matha Mnzava akiwa amesimama kujitambulisha kwa wajumbe wa Baraza muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa baraza hilo kulifungua rasmi.

 Bi.Emi Rweyendera kutoka CMA  ambaye amesimama akiwa anaendelea na zoezi la kugawa karatasi  kwa wajumbe za kupigia kura hiyo jana.

 Sehemu ya wajumbe wa Baraza wakingojea karatasi za kupigia kura muda mfupi kabla ya uchaguzi huo kufanyika,mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo jana asubuhi kuanzia saa tano.

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Wajumbe wapya watakao wawakilsha Wafanyakazi katika vikao vya Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia sasa. Uchaguzi huo ulisimamiwa na Bi.Emy Rweyendela kutoka Baraza la Usuruhishi (CMA) na Bi.Martha Mnzava kutoka TUICO Mkoa.

Friday, May 8, 2015

SEMINA YA UKIMWI & KIFUA KIKUU Sokoni Karikoo

 Katika picha hapo juu inaonesha muda mfupi kabla ya Semina kuanza ndani ya Ukumbi wa Shirika la Masoko Kariakoo siku ya Jumatano. Kutoka kulia wakwanza ni Dk.Leah Mtui wapili ni Bwana Chiziza Nelson wote wawili ni wafanyakazi kutoka shirika lisiliokuwa la Kiserikali linaloitwa PASADA, na watatu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Godwini Mrosso. Wote wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo pichani hayupo.
 Katika picha hapo juu ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya alipokuwa akitoa maneno ya kuwakaribisha Wawezeshaji wa semina pamoja na Watumishi wa Shirika waliohudhuria semina hiyo maalum. Meneja Mkuu huyo kama Mkuu wa Taasisi aliwaasa wanasemina kufuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyolenga kuwajengea uelewa zaidi kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na Kifua Kikuu.Semina hiyo ilifanyika siku mbili Jumanne na Jumatano, siku ya Jumanne semina hiyo iliwahusisha Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na siku ya Jumatano iliwalenga Watumishi wa Shirika.
 Meneja wa Idara ya Afya na Usafi wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Donald T.Sokoni akiwa anatoa ukaribisho kwa wanasemina kabla ya kuanza.Hii ilikuwa siku ya Jumatano asubuhi,na semina hiyo ilifanyika ndani ya Ukumbi wa Shirika hilo.
 Bwana Chiziza Nelson ambaye amesimama ni  moja ya Wawezeshaji wa semina hiyo iliyofanyika katika Shirika la Masoko Kariakoo siku ya Jumanne na Jumatano wiki hii. Semina ilikuwa ililenga kuwajengea ufahamu zaidi juu ya magonjwa mawili yakiwa ni Ukimwi na Kifua Kikuu.
 Bwana Nasoro Said mwenye shati la mistari akiwa anamsikiliza kwa utulivu kabisa Muwezeshaji wa Semina Dk.Leah Mtui kutoka shirika la PASADA pichani hayupo wakati anaendelea kutoa mafunzo yahusuyo ugonjwa hatari wa Ukimwi.
 Sehemu ya Wanasemina waliohudhuria wakiwa wameketi na kufuatilia kwa umakini sana mafunzo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa na wawezeshaji kutoka shirika lisilokuwa la Kiserikali liitwalo PASADA hii ilikuwa ni siku ya Jumatano wiki hii.
 Katika picha hapo juu aliyesimama ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya akitoa maneno ya shukrani kwa wawezeshaji wa semina iliyokuwa inahusu Ukimwi na Kifua Kikuu,mara baada ya kufikia mwisho wa mafunzo yaliyotolewa na Wafanyakazi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la PASADA.
Kazi na dawa kwelikweliii! Hapa katika picha ni sehemu ya Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanapata chakula mara baada ya kuhitimisha Semina maalumu iliyokuwa inahusu kuwajengea uelewa kuhusu magonjwa ya  Ukimwi na Kifua Kikuu.Semina hiyo iliyofanyika katikati ya wiki hii siku ya Jumanne na Jumatano katika ukumbi wa Shirika hilo ilikuwa yenye manufaa zaidi kwa Taasisi hiyo na mtu mmojammoja pia!

Wednesday, May 6, 2015

Kutoka Kariakoo Soko Kuu Jijini Dar Es Salaam

 Katika picha hapo juu ni sehemu ya Wajumbe wa kikao cha pamoja kati ya watumishi wa Shirika la Masoko Kariakoo wakibadilishana mawazo na Vijana wa kutoka Mtandao wa 2SEEDS Network ambao walifika sokoni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita kutemebelea soko hilo wakiongozwa na Bi.Anna ambaye katika picha anaonekana akifafanua jambo fulani katika kikao hicho.
 Picha hii hapo juu inaonesha sehemu ya Vijana wa 2SEEDS Network pamoja na Mkuu wa Kitengo cha ICT wakwanza kushoto Bwana Anderson Shaka, wakiwa wanafuatilia kwa umakini maelezo ya Afisa Biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Vedastus Valentine pichani hapo haonekani.
 Bwana Vedastus Valentine wa kwanza kulia akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao mwishoni mwa wiki iliyopita.Anayesikiliza kwa umakini karibu nae ni Bi.Ana LĂȘ Rocha ambaye ni Mkurugenzi wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania.

Katika picha hapo juu ni  Ujumbe kutoka Wilayani Mburu katika mkoa wa Manyara ulioongozwa na Afisa Biashara wa wilaya hiyo Bwana Jeremiah Mtagwa mwenye shati la rangi ya bluu waliposimama kujitambulisha katika kikao kifupi kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Shirika la Masoko Kariakoo
 Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikao,mara baada ya kumaliza kikao ndani ya ukumbi wa Shirika la Masoko Kariakoo.
Katika picha hizo hapo juu ni wajumbe waliohudhuria kikao cha kubadilishana mawazo jinsi ya kuendesha miradi mbalimbali.Katika picha hapo waliokaa kutoka kushoto wa kwanza ni Omary Mdakama  kutoka Kitengo cha ICT Shirika la Masoko Kariakoo,wapili ni Bwana Vedastus Valaentine, wa tatu ni Mkulima mkubwa wa vitunguu wilayani Mburu aliyeambatana na  Bwana Jeremiah Mtagwa ambaye ni  Afisa Biashara wa Wilaya ya Mburu mkoani Manyara ambao wote kwa pamoja walifika katika Soko la Kariakoo kuona na kujifunza mambo mbalimbali katika uendeshaji wa soko hili kubwa.