Tuesday, March 31, 2015
Samaki wa kila aina Sokoni Kariakoo
Kariakoo ni Soko kuu na kubwa sana hapa nchini Tanzania na hata katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki.Hupokea mazao ya kila aina kutoka mikoani na hata nchi jirani. katika picha hapo juu ni samaki wakavu ambao hawa huingizwa hapa sokoni kutoka Mkoani Morogoro hasa wilaya za Kilombero na Ulanga. Ukifika Sokoni Kariakoo samaki hawa wakavu wanapatikana eneo la Shimoni soko la samaki na dagaa. Samaki wa maji baridi na chumvi wote wapo hapo. Karibuni nyote katika Soko la Kariakoo!
Bidhaa zaongezeka bei Sokoni Kariakoo
Msimu huu nyanya zimepungua kwa kiasi kikubwa ,hii ni kutokana hali ya hewa kwa sasa ni mvua nyingi zinanyesha mikoani hivyo hata uzalishaji wake si mzuri. Kutokana na hali hiyo basi nyanya zimepanda bei kwa kiasi kikubwa! kwa kufikia sh.2000/= hadi 2500/= kwa kilo moja.
Monday, March 23, 2015
Wanawake na Maendeleo!!
Katika picha mbalimbali zinaonesha Wanawake kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa katika mapozi tofautitofauti siku ya tarehe 8Machi 2015 walipokuwa wakiadhimisha siku ya Wanawake Duniani wiki mbili zilizopita katika Viwanjavya Mnazimmoja Jijini Dar Es Salaam.
Wanawake wakiwa katika viwanja vya Mnazimmoja wakiendelea na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi 2015.
Mjasiriamali wa Vitunguumaji
Katika picha hapo juu ni mjasiriamali akiwa anachambua vitunguumaji kwa ajili ya kuuzia wateja wakifika hapo ubaoni kwake.Jina lake halikufahamika maramoja mapema leo asubuhi! Biashara ya vitunguumaji inafanyika kwa kiasi kikubwa eneo la Shimoni katika Soko hili. Vitunguu hivi hupatikana kwa bei ya jumla na rejareja. Karibu sokoni Kariakoo!
Friday, March 20, 2015
Bwana Shirazi ambaye ni Mfanyabiashara wa njegere alikutwa akizimeenya kama sehemu ya matayarisho ya biashara yake hiyo ili wateja wake wakifika aweze kuwapimia, bei ya njegere kwa Sokoni hapa Kariakoo ni kati ya Sh.6000/= hadi Sh.7000/= kwa kilo moja. Njegere ni miongoni mwa mazao ambayo huingizwa katika Soko Kuu la Kariakoo kila siku kutoka mikoni.
Wajasirimali Sokoni Kariakoo
Kariakoo eneo la Shimoni.
Thursday, March 19, 2015
Maarifa huongezwa kila siku
Katika picha hapo juu ni Meneja wa fedha Bi.Marieta Massaua na Bwana Peter Mshikilwa ambaye ni Mwanasheria, wote ni watumishi katika Shirika la Masoko Kariakoo. Hapo walikuwa wakihudhuria semina inayohusu Sheria ya manunuzi.Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo watumishi hawa jinsi yakutekeleza sheria hiyo muhim katika shughuli za manunuzi.
Kariakoo
Watumishi wa Kitengo cha Manunuzi Bwana Mathias Mbafu na Henrika Kawili wakijadili jambo kuhusiana na kazi zao za kila siku.Bwana Mathias Mbafu ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi.
Ndizi!Ndizi! sokoni Kariakoo
Friday, March 13, 2015
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana Florens Seiya akiwa anaongoza Mkutano baina ya Menejimenti ya Shirika na Wajumbe wa kamati kuu ya Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, walipokuwa wakijadili kuhusu wazo la kufanya maboresho eneo la maduka ya nyama(mabucha) ndani ya jengo kuu la Soko la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.
Thursday, March 12, 2015
Ushirikishwaji wa Wadau katika maendeleo ni muhimu
Katika picha hizo hapo juu ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam,wakiwa katika Mkutano wa pamoja na Uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo. Mkutano huo ulikuwa na agenda kuu moja tuu ya kuwashirikisha Wafanyabiashara hao katika wazo la kuboresha matumizi ya sehemu ya maduka ya nyama(Mabucha) iliyomo ndani ya jengo la Soko Kuu la Kariakoo, kwa nia ya kuliongezea tija shirika. Kwenye picha ya chini aliyevaa miwani ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya akifafanua jambo kwa Wajumbe waliohudhuria mkutano huo juzi, mkutano huu ulifanyika ndani Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.
Monday, March 9, 2015
Sokoni Kariakoo leo
Katika picha hapo juu ni moja ya wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo eneo la Shimoni ambaye yeye hufanya biashara ya matango na karoti. Hivi ndivyo alivyokutwa katika meza yake ya biashara mapema leo asubuhi.