Thursday, January 15, 2015
Nanasi ni Matunda bora kwa afya
Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam hupokea kila aina ya mazao. Katika picha hapo juu ni mananasi amabayo tayari yamefikishwa katika soko hili maarufu hapa Jijini Dar es Salaam. Mananasi haya huuzwa kwa bei ya jumula na rejareja sokoni hapo.
Nyanya zapanda bei sokoni
Mvua nyingi zinazoendelea katika mikoa maarufu ya uzalishaji nyanya imesababisha bei ya nyanya kupanda bei katika Soko Kuu la Kariakoo kwa nyanya grade ya kwanza.
Nyanya nyingi huingizwa katika Soko Kuu la Kariakoo kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Morogoro na Arusha.

Sunday, January 11, 2015
Kutoka Soko Kuu la Kariakoo
Katika picha hapo juu ni mjumbe akiwa anasaini daftari la mahudhurio katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi Chama Kikuu cha Ushirika cha Akiba na Kukopa SACCOS ambacho kinawashirikisha Wafanyakazi wa Shirika, kilifanya Mkutano muhimu wa kuwapata Viongozi wapya wa kukiongoza Chama hicho kwa muda wa miaka mingine mitatu.
Katika picha hapo juu ni baadhi tuu ya Wajumbe wapya wa Bodi ya SACCOS kutoka kushoto ni Bwana Yustino Man mwenye shati nyeusi,wapili ni Bwana Dennis Mfuruki na wa mwisho ni Bwana James Kanyiriri wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Soko kuu la Kariakoo.
Miongoni mwa Wajumbe (Wanachama) wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Kukopa Soko Kuu Savings LTD waliohudhuria mkutano maalum huo uliofanyika Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano. Mkutano huo ulikuwa na Agenda moja tuu ya kuwachagaua viongozi wapya wa Ushirika huo.
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi waliochaguliwa ni Bwana Bolingo Malya,Ncheye Kulwa Ncheye na Onesmo Sinziga
Bwana Godwin Mbuya akisaini akisaini karatasi maalumu ya mahudhurio aliyeshika karatasi kuhakiki jina la mwanachama huyo ni Makamu Mwenyekiti Bwana Mohamed Chikwama.
Mkutano huo uliwachagua Bwana Dennis Mfuruki,James Kanyiriri,Mohamed Chikwama,Yustino Man,Alphonce Mweri na Anderson Shaka Mjanga kuwa Wajumbe wa Bodi wa Saccos hiyo.

Tuesday, January 6, 2015
Mwaka 2015 Sokoni Kariakoo
Katika picha ni samaki wakavu ambao wanafikishwa katika Soko Kuu la Kariakoo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, kama vile mkoani Morogoro,Kilimanjaro na Iringa.Samaki hawa hupatikana kwa bei ya jumula na rejareja,tafadhali karibu ujipatie samaki hawa katika Soko Kuu eneo la Shimoni.
Mboga aina ya Kabichi kutoka Iringa,Mbeya,Tanga na kwingineko hufikishwa katika Soko Kuu la Kariakoo zikiwa zingali fresh kabisa kama inavyoonekana katika picha hapo juu.