Monday, October 13, 2014

Miongoni mwa Tunu za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere ambazo zingali zinaishi hadi leo!

 Ni miaka 15 tangu Baba wa Taifa alipotutoka Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla,lakini angali anaishi pamoja na Watanzania wa aina zote.Shirika la Masoko Kariakoo ni mojawapo ya Mashirika yaliyoanzishwa wakati wa uongozi wake mnamo mwaka 1974 kwa sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Soko Kuu la Kariakoo lilianzishwa maalum kwa ajili ya  Watanzania hasa wakulima na Wafanyabiashara wadogowadogo waendeshe shughuli zao hapa ili kuwakomboa kimaendeleo.Mwalimu alimjali kila mwananchi kwa nafasi yake.

 Katika picha hapo juu ni Soko Kuu la Kariakoo katika mwaka wa 1975 mara baada ya kufunguliwa rasmi na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius K. Nyerere.Wakati huu Soko Kuu la kariakoo lilikuwa na Wafanyabiashara kati ya 200 hadi 300, ambao walikuwa wakifanya biashara zao hapa.

 Hii ilikuwa ni tarehe 8/12/1975 Hayati  Mwalimu Julius K.Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaonekana akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.Ujenzi wake uligharimu kiasi cha Shilingi 22,000,000/=fedha za Kitanzania na pia lilijengwa na Wakandarasi wazawa tangu uchoraji na usanifu wa ramani kazi ambayo ilifanywa na Mhandisi Mzee wetu Beda Amuli nakujengwa na Kampuni ya MECCO kwa wakati. Jengo hili kwa sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya Sh.Bilioni 50.

Picha hii hapo juu inaonyesha watumiaji wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa wameongeza sana, hii ni miaka ya hivi karibuni. Wananchi wengi wakiwa wamejaa kupata mahitaji mbalimbali.

Tutakukumbuka daima kwani umetuachia Tunu za kila aina katika Taifa hili.