Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanatoka kwenda kupanda basi maalumu lililokuwa limekodiwa kwa ajili ya kwenda kutembelea na kukagua mali za Shirika. Aliyetangulia mbele ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe.Hii ilikuwa ni mojawapo ya agenda za kikao hicho cha Bodi.
Miongoni mwa Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakipanda basi tayari kwa safari kuelekea maeneo ya Mbezi Beach ambako ziko nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakiwa wamefika mahali zilipo nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo.Katika picha Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Wilson Kabwe akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano wa Bodi wakitembea kuelekea katika geti la nyumba mojawapo eneo la Mbezi Beach Makonde, huku wakiongozwa mbele na Afisa Usalama Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Josam Mnzava ambaye ameshikilia radio Call.
Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika wakiwa nje ya geti la nyumba mojawapo ya Shirika la Masoko Kariakoo,nyumba hizi zipo eneo la Mbezi Beach Mtaa wa Makonde.Anaye toa maelezo hapo ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya.Hii ilikuwa ni mwishoni mwa wiki liyopita.
Wajumbe wa Bodi ya ushauri walipata nafasi ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapo juu katika picha ni wajumbe hao walipokuwa eneo la Tabata bima Jijini Dar Es Salaam, ambako walifika kuona nyumba za Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam.Katika picha alikuwa akifungua Mkutano wa Bodi mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Tuesday, October 28, 2014
Monday, October 20, 2014
Wafanyabiashara wa Soko Kuu la kariakoo
Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa katika moja ya Masoko ya nje ambayo hufanyika Osterbay na Masaki jijini Dar Es Salaam siku za Jumamosi na Jumapili.Lakini pia katika Masoko haya huwashirikisha wakulima kutoka Wilaya ya Korogwe ambao husimamiwa miradi yao ya uzalishaji mali na matandao wa 2SEEDS Network.