Sunday, July 27, 2014

Maandalizi ya Sikukuu ya Idd katika mitaa ya Kariakoo

Watu mbalimbali Watanzania na wale wakutoka nchi jirani wakiwa katika pilikapilika za maandalizi ya sikukuu ya Idd.Maduka mengi yakiwa na bidhaa nyingi  mbalimbali ambazo zimekuwa na bei za wastani kama vile baadhi ya Wananchi walivyotoa maoni yao  mwishoni mwa wiki iliyopita.

Friday, July 25, 2014

KUREJEA KWA SOKO LA WAZI KATIKA VIWANJA VYA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO-DSM

 Picha hizi za michoro zote zinaonyesha mpangilio jinsi gani Maumbo yatapangiliwa kwa ajili ya Wafanyabiashara wa Soko la Wazi katika Viwanja vya Shirika la Masoko ya Kariakoo.Katika siku chache zijazo Wafanyabiashara hao watarejea  na kuanza kufanya shughuli zao za kibiashara.

Katika michoro hiyo inaonyesha vizuri maumbo zaidi ya miambili yatakavyopangwa na kuacha njia katikati kwa ajili ya kupita Wateja/Wanunuzi wa bidhaa. Eneo hili lipo kati ya Jengo Kuu la Soko na Soko Dogo.

Sunday, July 20, 2014

Mazao ya Mbogamboga

Pilipili hoho ni moja ya mazao ya mbogamboga ambayo huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.
Ukifika katika Soko Kuu la Kariakoo zao hili hupatikana Soko la Shimoni kwa bei ya jumla na rejareja. karibu upate huduma bora hapa Sokoni Kariakoo!

Wednesday, July 16, 2014

Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam akiendesha Mkutano wa Bodi hiyo jana Jumanne tarehe 15/7/2014.Mkutano huo maalum ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Mkutano huo ulipokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014; na hatimaye Bodi hiyo  ilipokea Bajeti mpya ya Shirika kwa mwaka  wa fedha 2014/2015 kuijadili na kuipitisha.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akiwakaribisha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri katika Mkutanoo huo maalum wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 na hatimaye kupokea na kuijadili na kuipitisha bajeti ya mwaka wa fedha  wa 2014/2015.Aliye upande wa kushoto mwenye shati  nyeupe ni Kaimu Meneja wa Biashara na Mipango wa Shirika bwana Mrero Mgheni.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi wakiwa Ukumbini bado wameketi Ukumbini mara baada ya Mkutano kumalizika.
Baadhi ya sehemu ya Wajumbe waliohudhuria  Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo jana Jumanne 15/7/2014.

Sunday, July 13, 2014

Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi

Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Shirika la Masoko wakiwa wanafuatilia taarifa zilizokuwa zikiendelea kutolewa katika mkutano huo wa baraza la Wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya  akiongoza mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.Kwa kawaida mkutano huo mkuu huhudhuriwa na Mjumbe mmoja wa TUICO kutoka Tuico ngazi ya Mkoa.

Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Godwin Mrosso mwenye shati nyeupe na Mjumbe wa TUICO Mkoa Bwana Willy Kibona kwa pamoja wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano walipokuwa wanahudhuria Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika  la Masoko ya Kariakoo.