Friday, January 31, 2014

PATA VITUNGUU SWAUM, KAROTI, HOHO KWA BEI POA KABISA SOKONI KARIAKOO


 mfanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salam Bwana Athumani Bungulumo akiwa katika meza yake ya biashara ya viungo vya chakula kama anavyoonekana hapo hapo juu pichani. bidhaa hizi unaweza kununua kwa bei kati ya shilingi 100/= na 200/=
Au unaweza kuweka oda ya bidhaa hizi kwa Mr. Athumani kwa mawasiliano yafuatayo.
0787 758222

Pata vitungu hapa kwa Daniel Maivaji Sokoni Kariakoo eneo la maarufu kama Shimoni. Je unahitaji bidhaa hizi? unaweza kununua Vitunguu swaumu kwa shilingi 6000/= kwa kilo pia Shilingi 4000/= tu kwa kilo moja ya tangawizio.
karibuni sana, 0755 231241 nipigie tufanye biashara. 

 Pata vitungu hapa kwa Munguatosha Sokoni Kariakoo eneo la maarufu kama Shimoni. Je unahitaji bidhaa hizi? unaweza kununua hoho kwa shilingi 1,000/= hadi 1,500/= kwa kilo moja
0752 884793 nipigie tufanye biashara
Hoho safi kutoka Kariakoo Soko Kuu Jijini Dar es Salaam- Tanzania

Monday, January 27, 2014

SOKO KUU LA KARIAKOO: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO KILICHOOHUSU MFUMO MPYA WA UTOAJI TAARIFA ZA MAZAO KUPITIA SIMU

 Wawakilishi wa Shirika la 2Seeds (Moniq Galvao wa kwanza kushoto na wa pili kulia Soph) wakiwa na Mwakilishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Anderson Shaka wa pili kushoto na Bariki wa kwanza kulia mwakilishi wa Habari Mazao) wakiwa katika kikao kilicho fanyika ndani ya ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Kikao hiki kilihusu Uboreshwaji wa mfumo wa utoaji taarifa za mazao kupitia simu ya kiganjani.

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kumalizika. kuazia wa kwanza kushoto waliosimama ni 
1. Anderson Shaka (Kariakoo Market)
2. Frank Mangowi  (Kariakoo Market)
3. Sugwejo Kaboda  (Habari Mazao)
4. Christian  (Habari Mazao)
5. Bariki  (Habari Mazao)
6. Soph (2Seeds Network)
7. Moniq  (2Seeds Network)

MAJADILIANO KUHUSU UUNDAJI WA MFUMO WA UTUNZAJI KUMBUKUMBU ZA SHIRIKA


Frank Tilugulilwa wa kwanza kushoto na Edward Mwangile kutoka katika kampuni ya  INCo yenye ofisi zake Sinza Jijini Dar es Salaam wakiwa katika kakao kilicho hushu namna ya uundaji wa Mfumo mpya wa utunzaji kumbukumbu za Shirika. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko ya Karikoo.


Afisa biashara wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bibi. Mwinga Luhoyo akiwa katika kikao cha Uundaji wa Mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu za Shirika.

MATUKIO KATIKA PICHA-KOROGWE

Katika picha hapo juu ni wawakilishi wa 2Seeds Network, Mfanyabiashara kutoka Soko Kuu la Kariakoo, Habari Mazao pamoja na Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Soko Kuu la Kariakoo wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kumaliza mkutano uliofanyika Korogwe Mkoani Tanga.


Katika picha hapom juu ni Anna ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la 2Seeds (Tanzania) kutoka Marekani lenye ofisi zake Tanzania akizungumza katika mkutano.


 Anderson Shaka Mjanga akizungumza kwa niaba ya Shirika la Masoko ya Kariakoo katika mkutano uliofanyika Wilayani Korogwe hivi karibuni.

Friday, January 24, 2014

SAMAKI KING FISH


Mfanyabiashara wa samaki katika maduka ya samaki ndani ya soko Kuu la Kariakoo akionesha samki aina ya King-fish ambaye anamuuza kwa shilingi 35,000/= lakini pia unaweza kupata vipande au ukapimiwa kwa kilo.

Tuesday, January 21, 2014

BCS - WAUZAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO CHA KISASA, WANAPATIKANA SOKONI KARIAKOO

Pichani hapo juu ni mifuko maalum ya kuhifahdia mbegu bora za nyanya, kama inavyoonekana hapo pichani. Mbegu hizi zimehifadhiwa katika mifuko yenye ujazo tofauti tofauti. Ipo ya Gram 10, Gram 25.  Mbegu hizi zinauzwa kwa bei ya Shilingi 5,000/= kwa mfuko.
Pichani hapo juu ni kopo maalum la kuhifadhia mbegu bora za bamia, kama inavyoonekana hapo pichani. Mbegu hizi zimehifadhiwa katika kopo yenye ujazo tofauti tofauti. Ipo ya Gram 10, Gram 25. Mbegu hizi zinauzwa kwa bei ya Shilingi 5,000/= kwa kopo

Huu ni mwonekano wa duka la BCS, Unaweza kuwasiliana nao kwa mawasiliano yafuatayo
+255 (0)754 272853
+255 (0) 787272 853
+255 (0) 715572 853



Monday, January 20, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA

Pichani hapo juu ni watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam, aliyesimama ni Mkuu wa Idara ya Usafi wa Shirika (Primitiva Kamugisha) na aliyekaa kulia kwake ni Afisa biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo (Bi. Soi) wakizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa sokoni Kariakoo (haonekani pichani) hivi karibuni katika ofisi ya Afisa biashara wa Shirika.

PATA BAMIA, NYANYA CHUNGU NA HOHO HAPA KARIAKOO SOKONI.

Friday, January 10, 2014

I.S & M (METALS) LIMITED

BUGGATI SPRAYER ZINAUZWA SHILINGI 25,000/=
 I.S & M Metals Limited ni wauzaji wa pembejeo za kilimo sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania.
Pichani hapo juu ni kifaa kinachotumika kunyunyizia dawa katika bustani na maeneo mengine.


 I.S & M Metals Limited ni wauzaji wa pembejeo za kilimo sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania.
Pichani hapo juu ni kifaa kinachotumika kunyunyizia dawa katika bustani na maeneo mengine.

Unaweza kuwapata I.S & M Metals Limited, Sokoni Kariakoo
Mawasilano yao ni: 0767 277473
                              0715 484444
                  Email: baly@intafrica.com




Wednesday, January 8, 2014

NAFAKA, MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZINAZOPATIKANA SOKONI KARIAKOO



MAHARAGE-SOKONI KARIAKOO


HOHO
Hoho zinazopatikana sokoni Kariakoo eneo maarufu kama Shimoni katika meza ya mfanyabiashara ya Munguatosha.

KUNDE
 Karibuni sokoni Kariakoo mjipatie bidhaa mbalimbali zikiwemo kunde na bidhaa nyinginezo nyingi.

Tuesday, January 7, 2014

KMC STAFF


Pichani ni baadhi ya watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye ofisi ya Afisa biashara mapema leo asubuhi.

SOKO LA WAZI KARIAKOO


Pichani hapo juu ni eneo la wazi la soko Kuu la Kariakoo ambalo ni maarufu kama soko la wazi, eneo hili unaweza kupata matunda na mboga mbalimbali kama vile nyanya, maembe, karoti, hoho, pilipili na mengine mengi.

Thursday, January 2, 2014

BEI YA SAMAKI YA PANDA KUTOKA SH.15,000/= HADI 16,000/= KWA KILO

Pichani hapo juu ni mteja wa samaki aliyefika katika maduka ya samaki wabichi ndani ya Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Samaki wanaoonekana pichani hapo juu wanauzwa Shilingi 16,000/= kwa kilo moja na shilingi 4,000/= kwa kipande.