Monday, November 4, 2013

PATA NYANYA, VITUNGUU PILIPIPLI, HOHO NA VINGINE VINGI SOKONI KARIAKOO KWA BEI POA


Wafanyabiashara wa eneo la wazi katika Soko Kuu la Kariakoo wakiendelea kufungua biashara zao mapema leo asubuhi. katika eneo hili unaweza kujipatia nyanya, vitunguu, pilipili, karoti, hoho, bamia kwa bei ya kawida na vitu vingine vingi kama inavyoonekana pichani



Mzani kwa ajili ya kupimia bidhaa ukiwa mezani tayari kwa kazi, ambapo baadhi ya bidhaa hupimwa kwa kilo.

Karoti safi na bora zinapatikana sokoni kariakoo, karibuni wote!!


Vitunguu kutoka Morogoro vinapatikana sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania


Pichani ni mfanya biashara maarufu wa vitunguu katika eneo la Kariakoo Shimoni, akiwa katiaka meza yake ya biashara kama picha invyoonesha hapo juu.


KING FISH: SAMAKI MTAM KUTOKA BAHARI YA HINDI


Tanzania tumejaliwa maliasili nyingi kuanzia nchi kavu hadi majini. Pichani hapo juu ni samaki aina ya King Fish ambaye amevuliwa katika Bahari ya Hindi Jijini Dar es Salaam, akiwa mezani sokoni Kariakoo tayari kwa kuuzwa.

Vipande vya Samaki kingfish vikiwa mezani kwa ajili ya kuuzwa, karibuni wote mjipatie samaki.


Geti kuu la kuingilia  Kariakoo Shimoni, ambapo magari kutoka sehemu mbalimbali nchini hupita katika mlango huu ili kuweza kupakua mzigo. Soko la kariakoo lililojengwa miaka ya 1970.