katika picha hapo juu ni Meneja wa fedha Mrs.Marieta Masaua akiwasilisha taarifa ya mapato ya Shirika,kushoto kwake ni Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi
Bwana Marco Mganga , Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi akifuatilia kwa makini maelezo ya Meneja wa fedha mapema leo asubuhi katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa mikutano.
Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ikiwa katika mkutano wake wa kawaida leo asubuhi! Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko.
Bi.Kamugisha Mkuu wa kitengo cha Usafi katika Shirika la Masoko ya Kariakoo akifuatilia jambo katika mkutano wa asubuhi mapema leo asubuhi.
NJOO KARIAKOO UJIPATIE SAMAKI WABICHI.
Pichani ni mfanya biashara maarufu wa samaki anayejulikana kwa jina la Bw Ramadhani Mlekwa anayefanya shughuli zake katika Soko kuu la Kariaoo. samaki wanaoonekana pichani ni aina ya "King fish"
Mteja akihakiki uzito wa samaki aliyemnunua kwa kupima katika mizani.Samaki hawa wanapatikana Sokoni kariakoo.
Baadhi ya wateja waliofika leo kununua samaki ndani ya Soko Kuu la Kariakoo kama inavyoonekana
pichani.Sokoni Kariakoo kila bidhaa hupatikana kuanzia Nafaka,Matunda,Viungo,Mbogamboga,Samaki na nyama
Wafanya
biashara wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiuza bidhaa zao kama
inavyoonekana pichani, katika soko la wazi. katika vipimo vya lita nne maarufu kama sado.Nyanya zinauzwa kati ya Sh.2000/= hadi Shilingi 3000/=kwa bei ya leo kwa sado
Biashara ya nyanya, karoti,hoho na nyinginezo mbalimbali hufanyika katika Soko kuu la Kariakoo kwa bei za rejareja na jumla. Katika hapo juu ni moja ya wafanya biashara mashuhuri sana hapa Sokoni akiwa katika meza yake! Karibuni wote mjipatie bidhaa safi na bora!!
Mawasiliano katika biashara ni mhimu! mama ambaye jina lake halikupatikana mapema akipanga bidhaa zake katika meza ya biashara huku akiwasiliana na wateja wake kama anavyooneakana katika picha.
Kitengo cha Usalama katika Shirika la Masoko ya Kariakoo
.
Katika picha hapo juu ni mtuhumiwa wa wizi wa simu akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa usalama wa Shirika la Masoko ya Kariakoo. (Jina lake limehifadhiwa)