Wednesday, October 30, 2013

Mtandao wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wang'ara.



Mtandao wa Shirika la Masoko ya Kariakoo- Tanzania  una speed ya kuridhisha katika kutoa huduma kwa jamii kama inavyoonekana hapo juu. load time ni sekunde 2.51 mtumiaji akiwa Texas kule Marekani, wadau waliopo huko wametujulisha! Lakini pia Mtandao huu umepimwa juzi tarehe 28/10/2013  Taasisi inayojishughulisha na mawasiliano kwa njia mtandao iliyopo Texas Marekani na matokeo yakawa kama yanavyoonekana hapo juu katika Picha. Website Speed Test  ilitoa alama kama zinavyo onekana hapo juu.

Tuesday, October 29, 2013

 Mchuuzi wa mizigo katika Soko Kuu la Kariakoo akitoka katika geti kuu la kutokea magari mara baada ya kushusha mizigo maarufu kama Shimoni, huku akiwa amebeba tenga la nyanya.

  Mchuuzi wa mizigo katika Soko Kuu la Kariakoo akitoka katika geti kuu la kutokea magari mara baada ya kushusha mizigo maarufu kama Shimoni, huku akiwa amebeba mkungu wa ndizi.

 Pichani hapo juu ni Afisa biashara wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Mwinga Mazwite Luhoyo  Mtumishi  akiwa ofisini.

JIPATIE NYAMA BORA SOKONI KARIAKOO

 
Pichani ni wafanyabiashara wa nyama katika Soko kuu la kariakoo wakiwa katika eneo lao la kazi kama inavyoonekana pichani. Ambapo nyama ya kawaida inauzwa Sh. 5000/= kwa kilo.


Jenga afya kwa kula Maini  bei yake Sh. 7000/= kwa kilo tu kwa takribani wiki hii!Sokoni Kariakoo unakamilisha mlo kamili kwa ajili ya familia yako kwa gharama ndogo tuuu! Karibu  sanaaa!






 Bwana Fadhili Rashidi akiwa katika sehemu yake ya biashara ndani ya Sokoo Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam. kwa mahitaji ya nyama unaweza kumpata kwa mawasilianop yafuatayo. 0754 418469




Nyama aina ya beef stake inayouzwa Sh. 7000/= kwa kilo;bei hii kila mmoja wetu anaweza kumudu kujipatia kitoweo!

Monday, October 28, 2013

KMC-Staffs

 Meneja Utumishi Msaidizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bw. Charles Sombe akiendelea na majukumu yake ya kila siku ofisini kwake.




Watumishi wa Shirika la Masoko Bi.Ikunda Mambo anayesoma gazeti na Saum Kiula wakiwa ofisini mapema leo  Jumatatu asubuhi.







Pichani hapo juu ni baadhi ya bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani zinapatikana Sokoni Kariakoo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la soko la wazi katika Soko Kuu la Kariakoo, hapa unaweza kupata karoti, tango, Pilipili hoho, nyanya chungu  n.k. vikwa freshiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! kabisa

 MUSYANGI HERBALISTIC CLINIC & RESEARCH CENTER


Elias Samweli Mtoa huduma wa Musyangi Herbalist Clinic & Research Center
Pichani hapo ni watoaji wa tiba asilia kwa Magonjwa mbalimbali ya binadamu; pia wanatoa ushauri na utafiti wa dawa za asilia. sasa wapo Sokoni Kariakoo

Friday, October 25, 2013

BEI YA VITUNGUU YASHUKA SOKONI KARIAKOO, KUTOKA Sh 150,000/= HADI Sh. 70,000/= KWA GUNIA

Pichani ni magunia ya vitunguu yaliyopo katika soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, vitunguu sokoni Kariakoo vimeshuka bei hadi kufikia bei kati yaSh. 800/= na 1,000/= kwa kilo, ambapo gunia la vitunguu kwa sasa linauzwa Sh. 70,000/=  kutoka Sh. 150,000/=

Mtakwimu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Ndugu Henry Rwejuna akiwa na Mratibu wa Mradi wa Masoko Monique Galvao wakiendelea na shughuli zao katika moja ya maeneo ya kuuzia vitunguu Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.


Pichani hapo juu ni mfanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo ambae jina lake ni Jackson Atanas Kibwe akipanga vitunguu katika meza yake ya biashara Sokoni Kariakoo. Jackson ambae ni mfanyabiashara maarufu sokoni hapa anapatikana kwa mawasiliano yafuatayo; 0712 834355

Shaban Muhud Saro (kulia) akiwa na watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo mapema leo asubuhi, ambapo Mtakwimu wa KMC alipofika mezani kwake. Shaban Muhud Saro ambaye pia ni mfanyabiashara wa vitunguu Sokoni Kariakoo amelipongeza Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kuanzisha mtandao wake ambao utasaidia kutoa taarifa mbalimbali zinazopatikana sokoni Kariakoo. Lakini pia Shaban Muhud Saro ametoa mawasiliano yake kwa yeyote atakaye hitaji huduma yake anapatikana kwa simu 0655 358343 au 0688 943368

Karibuni ujipatie vitunguu Sokoni Kariakoo


Wednesday, October 23, 2013

YALIYOJILI KATIKA HARUSI YA MKUU WA KITENGO CHA ICT -KARIAKOO


Muda mfupi kabla ya kuanza ibada ya ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam;kutoka kushoto ni Bwana harusi Anderson Shaka Mjanga na bestman wake bwana Aron Mjema,wengine ni Frank Mangowi mfanyakazi wa kitengo cha ICT KMC na mwingine ni Kamili Simba pia mfanyakazi wa KMC


Muda mfupi kabla kufunga ndoa Bwana Harusi na Best Man wake wakiwa katika viwanja vya kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. Hii ilikuwa Jumamosi  ya tarehe 19/10/2013

Bwana na Bibi harusi wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa yao Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha Matarumbeta cha Kanisa la KKKT Kijitonyama jijini DSM kikitumbuiza kanisani hapo mara baada ya Bwana Anderson Shaka Mjana Na Bi Neema Elibariki Mshanga kufunga ndoa yao kanisani hapo Jumamosi ya tarehe 19/10/2013. Bwana harusi ni Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo na Bibi harusi ni Mjasiriamali.

 
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa  mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam,Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.

Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wa pande zote mbili yaani familia ya Mzee Mjanga na Mzee Mshanga;mara baada ya vijana wao kufunga ndoa jumamosi ya tarehe 19/10/2013, kanisani Kijitonyama KKKT.

Ndugu wa Bwana harusi wakifurahia mara baada ya Ibada ya kufunga ndoa kumalizika kati ya Bwana Anderson Shaka Mjanga na Bi Neema Elibariki Mshanga KKKT pale Kijitonyama.Mwenye suti kushoto ni mdogo wake na Bwana harusi Daktari S.Mjanga toka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro;na mwingine ni binamu yake na Bwana harusi.
Muda mfupi baada ya Bwana Anderson Shaka Mjanga  kufunga ndoa  na Bi Neema Elibariki Mshanga.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.Ndoa ilifungwa katika kanisa la KKKT Kijitonyama na baadaye tafrija fupi kufanyika katika Ukumbi wa Dolphin 1998 LTD uliopo Sinza karibu na S/Msingi Mugabe.kutoka kushoto ni Everine,Erica,Amina,Munira na Joyce.

  Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.


PATA BIDHAA BORA KUTOKA SOKO LA KARIAKOO

Pichani ni Mhasibu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) Bw. Ibrahim Marsha aikwa ofisini kwake hivi karibuni. katika mahojiano yaliyofanywa baina ya mchambuzi wa maswala ya ICT ya Shirika la Masoko ya Kariakoo (Frank Mangowi) hayupo pichani. Marsha alielezea historia fupi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, bofya hapa ili kupata historia ya Shirika la Masoko ya Kariakoo.




Aidha Marsha anachukua nafasi muhimu kuwakaribisha wateja kujipatia bidhaa mbalimbali zinazopatikana sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Hapa ndipo Kariakoo Sokoni, picha ikionesha Soko kubwa(kushoto) na Soko dogo(kulia) la Kariakoo jijini Dar es Salaam.




Monday, October 21, 2013

PEMBEJEO ZA KILIMO ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO




Wakati serikali ikiweka jitihada nyingi katika kuinua uchumi nchini (KILIMO KWANZA), kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha, wafanya biashara pia hawako nyuma, wengi wao hapa nchini wamekuwa wakiuza pembejeo za kilimo cha kisasa kama inavyoonekana katika picha. Mfanya biashara () aliyepo ndani ya soko Kuu la Kariakoo (KMC) akionesha mfuko wa dawa “Ivory M 72 wp” inayosaidia kuondoa ukungu,fangasi  katika mimea mbalimbali kama mua, mboga za majani nk.
Miongoni mwa bidhaa zinazopatika ni pamoja na mbegu za Arizeti, mbegu za maboga, mahindi, figiri mchina na nyinginezo nyingi.
Pichani ni miongoni mwa mbegu za kisasa za mazao mbalimbali zinazopatikana dukani  “ZAWADI AGROVET” lilopo ndani ya soko kuu la Kariakoo-Dar es salaam.
Simu :0764 534005 au 0716 931940.



Friday, October 18, 2013

JIPATIE PILIPILI, VIAZI, VITUNGUU KWA BEI NAFUU SOKONI KARIAKOO


Jipatie pilipili

Wafanya biashara wakiwa kwenye harakati za kuandaa bidhaa zao kwa ajili ya biashara mapema leo asubuhi.


Wafanya biashara wakiwa kwenye harakati za kuandaa bidhaa zao kwa ajili ya biashara mapema leo asubuhi Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Thursday, October 17, 2013

Maonesho

Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi (katikati) akizungumza na wawakilishi wa Kikundi cha MUDA Afrika sambamba na wawakilishi wa UN hivi karibuni. MUDA Afrika walihitaji kupewa nafasi watakayo fanyia shughuli zao za maonesho kwa muda wa siku mbili katika eneo la Soko Kuu la Kariakoo.
_______________________________________________________________________

Pichani Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi akiendelea na mazunguzo na wawakilishi wa MUDA Afrika.
_____________________________________________________________________

Tuesday, October 15, 2013

KIBA INVESTMENT: WAUZAJI WA VIUNGO VYA PILAU SOKONI KARIAKOO




Pichani ni baadhi ya viungo vya pilau vinavyo patikana katika duka la KIBA INVESTIMENT, duka lililopo Sokoni Kariakoo.
Vitunguu maji

vitunguu swaumu

Mr. Kiba,  mmoja ya wafanya biashara maarufu sokoni kariakoo akiwa dukani kwake mapema leo asubuhi.

HEKA HEKA ZA SIKU KUU YA IDD EL HAJJ

Wateja wakijipatia mahitaji yao sokoni Kariakoo kama inavyoonekana hapo juu pichani, hili ni eneo la wazi la Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Nyanya, vitunguu, hoho karoti zapatikana kwa wingi Sokoni Kariakoo.
Njegere
Katika harakati za siku kuu ya Id-Elhaj baadhi ya bidhaa zapanda bei, baadhi ya bidhaa hizo ni kama vile njegere.

Baadhi ya bidhaa ambazo zimeonekana kupatikana kwa wingi sokoni Kariakoo ni pamoja na nyanya, vitunguu maji & swaumu.



Pichani ni mfanya biashara wa Soko Kuu la Kariakoo eneo la Soko la wazi Merck Wandao Twanga  ambae pia ni Mwenyekiti wa wafanya biashara wa eneo la wazi sokoni Kariakoo.




Jipatie karoti, hoho, tango