Baada ya
vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuisha mwaka 1919 na nchi yetu kuanza kutawaliwa na
Waingereza , jengo hilo lilianza kutumika kama Soko na kuhudumia wakazi a mjii
huu. Wakati huo wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sakafuni kwa sababu
hapakuwa na meza. Wafanya biashara waliendelea kufanya biashara sakafuni hadi miaka ya 1960 wakati
meza za saruji zilipojengwa. Kwa kadri Jiji la Dar es Salaam lilivyokua na
wakazi wake kuongezeka, ndivyo Soko hilo la zamani lilivyokuwa
likishindwa kumudu kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Pamoja na kubanana katika
soko hilo na biashara kufanyika katika mazingira yasiyoridhisha, pia halikuwa
na ghala za kuhifadhia bidhaa. Hali hiyo iliwafanya viongozi wa Halimashauri
ya Jiji kuona haja ya kuwa na soko kubwa na la kisasa kulingana na maendeleo ya
Jiji na hivyo wakaanza kujadili uwezekano wa kujenga soko jipya.
Uamuzi wa
kujenga Soko Kuu la Kariakoo la sasa, ulifanywa na Serikali mnamo mwaka 1970
baada ya majadiliano yaliochukua muda baina ya Serikali kuu na Halmashauri ya Jijikama wadau ili kuweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa Jiji la dar Es Salaam.
Serikali
iliagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kujenga Soko
jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya Soko la zamani lililokuwa hapa
Kariakoo.
Matarajio ya
uamuzi huu wa serikali wa kujenga Soko jipya yalikuwa ni kuwapatia wakazi wa
Jiji mahali au Soko kubwa ambalo lingetosheleza mahitaji yao kwa muda wa miaka
50 hadi 70 ijayo kuhusu mambo yote ya vyakula, yaani uuzaji jumla , mahala pa
kuhifadhi vyakula na uuzaji wa rejareja.
Mipango yote
ilikamilika na ujenzi ulianza rasimi mwezi Machi 1971. Ramani ya jengo la Soko
ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo Injinia Mtanzania Mzalendo kabisa Ndugu
Beda J. Amuli ambaye anaishi hapa Jijini Dar es Salaam hadi sasa. Wajenzi waliojenga jengo la Soko ni Mwananchi
Engineering and Contracting Company (MECCO) wakisaidiana na Wakandarasi wengine
kadhaa kwa kazi mbalimbali zilizohita wataalam maalum. Shughuli zote za ujenzi
zilikamilika mwezi Novemba 1975, na Soko lilifunguliwa rasmi kwa matumizi ya
wananchi hapo tarehe 8 Desemba, 1975 na Mwlimu Julius K. Nyerere,aliyekuwa Rais wa kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpaka kukamilika, ujenzi wa Soko ulighalim
jumla ya shilingi za Kitanzania 22 milioni.
Pia machapisho yanayo lielezea soko hili kubwa la kariakoo yanaelezea kuwa Mkandarasi ndugu Beda J. Amuli kabla ya kuanza kazi yake aliagizwa na Hayati Mwl.Julius K.Nyerere wakati huo akiwa rais wa nchi hii kuwa asafiri kwenda Accra-Ghana na Lusaka-Zambia,huko alikwenda kujifunza Study tour kuhusu masoko yaliyokuwa tayari yamejengwa katika miji hiyo miwili na ndipo atengeneze ramani yake kwa ajili ya ujenzi wa soko hili ambalo tunaliona leo.
Mkandarasi Mzalendo alifanya hivyo na hatimaye kuja kutoka na ramani hii ya jengo letu ambalo kimsingi kuna baadhi ya muonekano(Features) zipo katika masoko hayo mawili toka nchi hizo mbili; na baadhi ni za kipekee kabisa ambapo hata ukienda Lusaka -Zambia au Accra Ghana hutazikuta. Hii ndiyo sifa pekee inayolifanya Jengo hili la Soko kuu la Kariakoo kuwa la tofauti na masoko mengine katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati pia.

SOKO KUU LA KARIAKOO
Soko la
kariakoo lipo katikati ya eneo la Kariakoo katika kiwanja Na. 32 Zone III na
limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikuku na Tandamti. Soko lina
majengo mawili ambayo yameunganishwa katika ghorofa ya chini ya aridhi. Majengo
haya mawili pamoja na sehehem inayounganisha ya eneo lenye jumla ya mita
17,780. Jengo la kwanza linaweza kuitwa
Soko Kubwa na jengo la pili Soko dogo. Soko kubwa limegawanyika katika sehemu
tatu ambazo ni ghorofa ya kwanza, ghorofa ya katikati na ghorofa ya chini
(Basement). Soko dogo ni soko la rejareja ambalo si tofauti na masoko mengineya
Jiji la Dar es Salaam.
Asante kwa makala nzuri kuhusu soko hili. ni muhimu 'kudocument' majengo yetu tena yale ya kihistoria na ya kuvutia
ReplyDeleteVipi kuhusu Kodi za wakati huo, na kwanini halikarabatiwi
ReplyDeleteSoko letu limeungua basi roho inauma sana
ReplyDeleteLoo solo letu limeungua. Na majengo mengi has a madhule yanaendelea kuungua. IPO haja serikali yetu kuja na jibu moja la kubaini kama ni hujuma za makududi au la ., na ichukue hatua Kali ili kama ni hujuma za aina hii adhabu ziwe wazikwa wote na Kali ili zisijirudierudie kwani ni hasara na majonzi kwetu watanzania.
ReplyDeleteNi kweli Soko Kuu la Kariakoo liliungua! Lakini tayari Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekwisha kutoa zaidi ya Sh.26 Bilioni, kwa ajili ya kufanya ukarabati wa Jengo la Soko Kuu, pamoja na Kujenga Jengo lingine litakalokuwa na ghorofa 8 sehemu ambapo lilikuwepo Soko dogo. Na Kazi inaendelea sasa, Mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati.
ReplyDeleteinterested.
ReplyDelete